MPANGO NA AGIZO LA MUNGU KWA MKE
by Jane Lawi Sijaona on Saturday, October 1, 2011 at 12:48am
BIBLIA inatoa agizo kwa mke kuwa MTII kwa mume wake.
Ninyi wake watiini waume zenu kama kumtii BWANA YESU. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama KRISTO naye ni kichwa cha Kanisa, naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo KRISTO, vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Waefeso 5:22-24.
Enyi wake watiini waume zenu kama ipendezavyo katika BWANA. Wakolosai 3:18
Kadhalika ninyi wake watiini waume zenu, kusudi ikiwa wako wasioamini NENO wavutwe kwa mwenendo wa wake zao pasipo lilo NENO. 1Petro 3:1 Ninyi wake watiini waume zenu kama kumtii BWANA YESU. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama KRISTO naye ni kichwa cha Kanisa, naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo KRISTO, vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Waefeso 5:22-24. Enyi wake watiini waume zenu kama ipendezavyo katika BWANA. Wakolosai 3:18 Kadhalika ninyi wake watiini waume zenu, kusudi ikiwa wako wasioamini NENO wavutwe kwa mwenendo wa wake zao pasipo lilo NENO. 1Petro 3:1
1. MAANA YA UTII
Utii ni kujiweka wewe mwenyewe chini ya mamlaka iliyo halali. Kibiblia ni, kwanza, kuutambua na kuukubali muundo wa mamlaka aliouweka MUNGU, na pili, kukubali kuwa chini ya mamlaka hiyo.
Kuna mambo matatu ya msingi yanayotokana na neno utii:
i) Hili ni agizo na sio maoni au mawazo
ii) Ni jambo la kila siku katika maisha ya ndoa
iii) Ni jambo ambalo linatakiwa litoke ndani ya mke mwenyewe, sio kwa shinikizo ua kulazimishwa toka nje.
Kumbuka kuwa MUNGU alimuumba Hawa kuwa msaidizi wa Adamu. Hivyo ana nafasi yake kwa Adam katika ndoa na familia kwa ujumla. Ukisoma Mithali 30:10-31 utaona aina ya mke ambaye anatakiwa kupigiwa mfano.
- ni mwenye thamani kubw kwa mumewe na hazina ya familia
- ni mchapa kazi hodari na anasaidia famila yake kimaisha
- ni mwenye hekima, anaifunza vyema familia yake na maisha bora ya kumcha MUNGU
- ana hofu ya MUNGU na anaishi maisha ya kumtii YEYE.
2. IMANI POTOFU
MUNGU anawaheshimu wale wote ambao kwa kutumia uhuru wao wa maamuzi huamua kumtii yeye na sio wale wanaodandia haki sawa.
3. MIPAKA KATIKA UTII
Wakolosai 3:18 Ninyi wake, watiini waume zenu kama ipendezavyo katika BWANA.
Waefeso 5:22 Enyi wake, watiini waume zenu kati kumtii BWANA wetu.
Hapa tunaona Mtume Paulo anaonyesha kuwa MUNGU hahitaji utii wenye upofu. Mke haruhusiwi kamwe kufuata uasi wa mume wake yaani kwenda kinyume na matakwa ya BWANA.
0 comments:
Post a Comment