Biblia inatufundisha kuhusu maisha ya ndoa kwa ukamilifu ila tunaishi katika dunia iliyoanguka na kugubikwa na dhambi.
I. UKWELI: BIBLIA INAFUNDISHA NINI KUHUSU NDOA MSETO
1. Mkristo asioe/kuolewa na mtu asiyeamini – 1Wakorintho 6:14-18.
Agizo hili linawagusa wakristo ambao si wanandoa. Usikubali kuoa/kuolewa na mtu ambaye si mkristo. MUNGU anaputuambia tusifanyed jambo fulani huwa ana makusudi maalum na sisi. Mpango wa MUNGU katikaqq ndoa ni kutupatia mwenza (Mwanzo 2:18) ambaye tunafanana naye n ambaye tutakuwa mamoja kimwili, kihisia na kiroho. Watu wengi wanapata matatizo kwa sababu wamelipuuzia agizo hili la MUNGU.
2. Mkristo asimuache mume/mke asiyeamini – 1Wakorintho 7:12-14.
Agizo hili linawagusa wakristo ambao wamehaingia katika ndoa mseto. Kwa mapenzi ya MUNGU ujitahidi kufanya kila uwezalo ili kujiletea mafanikio katika hali uliyonayo. Hii inamaanisha kwamba usisitishe mahusiano. Usimkoseshe raha mwenzi wako kwa kumfanyia vituko ili aondoke. Kwa neema ya MUNGU inawezekana kwa jitiuhada zako ,kristo ukamuongoa mwenzi wako.
Iwapo asiyeamini ataamua kuondoka anayeamini hana hatia – 1Wakorintho 7:15-16.
Pamoja na jitihada zote ambazo anazifanya ili kudumisha mahusiano, asiye mkristo akuamua kuondoka ni hiari yake mwenyewe kwani maandiko yanasema “Lakini Yule asiyeamini akiondoka na aondoe. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini MUNGU ametulia katika amani”.
II. BUSARA/HEKIMA: JINSI YA KUISHI NA WATU WASIOAMINI
Busara ni ufunguo wa kumuongoa asiyeamini na kumleta kwa KRISTO, yaani unatumia akioli kutekeleza jambo pasipo uadui. Ukiwa umeshaingia kwenye ndoa mseto ni jitihada gani unazozifanya ili ufanikiwe? Je atamwalika mwenzi wako kanisani kila siku na kuongea naye habari za Bblia? Soma 1Petro 3:1-7
1. Ishi katika vitendo na sio maneno
Katika aya ya kwanza Mtume Petro anawaambia wake ambao waume zao sio wakristo njia nzuri ya kuwavuta ni mwenendo wao na sio porojo. Katika kushuhudia ni lzima kuwe na uwiano kati ya maneno na matendo. Hapo utagundua kuwa kanuni ni zile zile kama kwenye wanandoa ambao wote ni wakristo. Kwa maneno mengine, mchukulie mwenzi wako kama unavyomchukulia mkristo mwenzako.
2. Wake, watiini waume zenu – 1Petro 3:1
Njia pekee ya mke kumshuhudia mumewe ni utii ambao unaonyeshwa kwa vitendo. Mke aishi maisha yenye mwenendo safi toka ndani.
3. Waume, wapendeni wake zenu – 1Petro 3:7
Hapa tujifunze kitu kimoja muhimu. Kamwe mume hatoweza kumuongoa mkewe kama atakuwa katili, mbinafsi na dikteta. Anachotakiwa kufanya ni kumpenda mke wake kama KRISTO anavyolipenda Kanisa lake.
III. UAMINIFU
Inawezekana umeyafanya yote ambayo Mtume Paulo ameagiza (1Petro 3:1-7) lakini hakuna mabadiliko yoyote nap engine mambo ynazidi kuwa mabaya zaidi; utafanyaje?
1. Jaribu kujichunguza mwenyewe maisha yako. Inawezekana kuna tatizo mahali. Jitahidi kuishi maisha yanayostahili mfuasi wa YESU KRISTO kuishi. Hakikisha kwa namna yoyote huwi kikwazo kwa mwenzi wako.
2. Uvumilivu. Ni jambo la msingi sana katia maisha ya ndoa kwani ndio siri ya mafanikio. Kumuongoa mwenzi wao si jambo la siku moja kama vile unavyowahubiria watu katika mikutano ya hadhara na kuwaambia walio tayari kumpa YESU maisha yao wanyoshe mikono ama wapite mbele. Ni jambo ambalo linahitaji muda na uvumilivu mwingi.
3. Inawezekana mume/mke amefanya yote hayo lakini hakuna mafanikio ya aina yoyote, achana nnaye. Wakati pekee ambao mkristo anaweza akafikiria suala la kuachana na mwenzi wake ni pale ambapo anaona sasa mahusiano yao yanawapeleka pabaya na uathiri familia au watoto. Hata hivyo kabla ya kuchukua hatua hiyo jaribu kutafuta msaada toka kwa wakristo waomavu kiroho hasa wazee wa Kanisa. Ikiwa wazee nao wataona kuwa mambi ni magumu na haiwezekani, uamuzi wa kuchana na mumeo/mkeo asiyeamini utakuwa sahihi.
BARIKIWA Posted in: QUOTES Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment